Waziri mkuu wa Ugiriki Alexis Tsipras amesisitiza taifa hilo lina fedha za kutosha kuendesha majukumu yake huku serikali yake ikijandaa wiki hii kujaribu kulipa sehemu ya madeni yake kwa wakopeshaji wake. Tsipras amewaambia wanahabari baada ya kukutana na waziri wake wa fedha Yanis Varoufakis hapo jana kuwa hawana tatizo la kupata fedha. Hayo yanakuja huku Ugiriki ikipanga kulipa euro bilioni moja siku ya Jumatano kama sehemu ya kupunguza mzigo wa madeni yake kuambatana na masharti ya wakopeshaji wake shirika la fedha duniani na Umoja wa Ulaya. Ugiriki haijaweza kupata mkopo wa kuukwamua uchumi wake kwasababu serikali mpya bado inafanya mazungumzo na wakopeshaji kuhusu mpango wake wa kufanya mageuzi ya kiuchumi ili kutimiza masharti ya mikopo zaidi.Varoufakis amesema matatizo madogo ya fedha hayapaswi kuligawanya bara la Ulaya.
16 Machi 2015 - 11:54
Msimbo wa Habari: 677175
Waziri mkuu wa Ugiriki Alexis Tsipras amesisitiza taifa hilo lina fedha za kutosha kuendesha majukumu yake huku serikali yake ikijandaa wiki hii kujaribu kulipa sehemu ya madeni yake kwa wakopeshaji wake.